Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (Mbeya UWSA) ni miongoni mwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanzania Bara. Mamlaka ilianzishwa mwaka 1998 kwa Sheria Na. 8 ya 'Water Works Act Cap 272' ya mwaka 1997, iliyofanyiwa marekebisho na Sheria Na.12 ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2009. Mamlaka ya Majisafi Mbeya imepatiwa daraja "A".
Mamlaka ya daraja "A" inawajibika kugharamia shughuli za uendeshaji, matengenezo, mishahara na kuchangia asilimia 15% ya mapato yake kwenye shughuli za maendeleo. Mamlaka ina dhamana ya kutoa huduma bora ya majisafi pamoja na usafi wa mazingira kwa wakazi waishio Jiji la Mbeya na Mji wa Mbalizi iliyopo Kusini Magharibi mwa Tanzania. Miji hii inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 630,000 (Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022).
DIRA (VISION)Kuwa mamlaka bora kwa kutoa huduma bora na endelevu ya majisafi na usafi wa mazingira ifikapo 2025.
DHIMA (MISSION)Kutoa huduma bora na endelevu ya majisafi na usafi wa mazingira kwa wakazi wa Jiji la Mbeya na Mji wa Mbalizi kwa bei himilivu.
KAULIMBIU (SLOGAN)'Maji ni Uhai'
MKURUGENZI MTENDAJI CPA. Gilbert Kayange
KURIPOTI MIVUJO NA WIZI WA MAJI
Ili kuripot mvujo wa maji (Mfano: bomba kupasuka n.k), kuripoti wizi wa maji au uharibifu wowote wa miundombinu ya maji, tafadhali piga simu ya Ofisi namba: 0800110088 bure.
GALLERY