• Toll Free: 0800110088
  • Box: 2932, Sinde Area - Mbeya Tanzania

Kitengo cha Huduma kwa wateja (Call center)

Utangulizi

Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Mbeya ilianzisha kitengo cha Huduma za dharura kwa wateja (Call center) mwezi Agosti 2019 lengo likiwa kuwahudumia wateja kwa ukaribu zaidi. Kupitia kitengo hiki wateja wanapata huduma moja kwa moja ya msaada wakiwa nyumbani au popote kwa njia ya simu ya mkononi.

Shughuli / Kazi katika kitengo

Baadhi ya kazi zinazofanywa na kitengo hiki ni pamoja na:-

  1. Kutoa taarifa kwa wateja kama kuna hitilafu za maji / kukosekana kwa huduma katika maeneo husika
  2. Kuelemiksha wateja namna sahihi ya kufanya malipo ya maji
  3. Kupokea Maoni / Malalamiko ya wateja na kuyawasilisha katika idara husika ili yashughulikiwa na mteja kupatiwa majibu
  4. Kupokea taarifa mbambali kutoka kwa wateja kama za kuhusu mivujo, wizi wa maji
  5. Kushughlikia wateja ambao wanakua hawajapata ankara zao za maji kwa sababu mbalimbali.

Muda wa kufanya kazi

Kitengo cha huduma kwa wateja kinafanya kazi kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 4 usiku. Lengo likiwa ni kufanya kazi mpaka masaa 24 ya siku. Hivyo mteja kwa sasa atapiga simu ya bure na kupata huduma kwa muda huo.

Namba ya kupiga simu bure

Namba ya simu ya bure ni: 0800110088