• Toll Free: 0800110088
 • Box: 2932, Sinde Area - Mbeya Tanzania

Majibu kwa Maswali ya mara kwa mara

Ili upate kuunganishwa na huduma ya majisafi/majitaka inakupasa kufika katika ofisi za Mamlaka ya maji kuchukua na kujaza fomu bila gharama yoyote. Mteja anaweza kupakua fomu ya maombi kwa kubonyeza hapa. Kisha wataalamu wa Mamlaka watafika katika eneo la mteja na kupima umbali aliopo mteja kutoka kwenye bomba kuu la maji. Mteja atajulishwa orodha ya vifaa vinavyohitajika na kuelekezwa kuvinunua ili aunganishiwe huduma ya maji.

Mteja anaweza kulipia ankara ya maji kwa mawakala wote wa Benki za Posta, NMB, NBC, na CRDB na Kupitia mitandao ya simu kwa huduma za MPESA, AIRTEL MONEY, TTCL PESA, EASY PESA, na HALOPESA. Ili kuweza kufanya malipo, ni lazima kuwa na Namba ya Malipo (Control Number) ina tarakimu kumi na mbili (Mfano: 994550451254). Kulipa kwa simu fuata hatua hizi:-

 1. Bonyeza: *150*00# ili kuingia kwenye menyu ya MPESA (Mitandao mingine fuata code namba husika)
 2. Bonyeza namba 4 (Lipa kwa Mpesa)
 3. Bonyeza namba 5 (Malipo ya Serikali)
 4. Bonyeza namba 1 (Weka namba ya Malipo)
 5. Ingiza namba yako ya Malipo (Mfano: 994550451254)
 6. Ingiza Kiasi
 7. Ingiza namba yako ya Siri ili kuthibitisha malipo kwenda MBEYA WSSA
AU:
 1. Bonyeza: *152*00# Kwenye simu yako
 2. Bonyeza namba 6 (Maji)
 3. Bonyeza namba 1 (Huduma za maji za pamoja)
 4. Bonyeza namba 3 (uliza Deni)
 5. Ingiza Akaunti namba yako ya maji (Mfano: A45500178012)
 6. Utapata deni lako
 7. Chagua 1 ili kulipa moja kwa moja
 8. Utapelekwa kwenye sehemu ya ingiza namba ya Siri ili kufanya malipo
Kwa msaada zaidi tafadhali piga simu ya ofisini bure kwa namba: 0800110088

Ikitokea mteja hapati bili ya maji kwa njia ya meseji itakua ni tatizo la mtandao (network) hivyo mteja naombwa kuangalia bili yake kwa kuingia kwenye tovuti ya mamlaka kubonyeza kwenye menyu ya ankara na kufuata maelekezo. Au anaweza piga simu ya bure (0800110088) na kuuliza ankara yake. Au kwa bonyeza hapa Angalia ankara

Dira inashindwa kusomwa na wasomaji kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwamba dira inakua imefungiwa ndani ya uzio wa nyumba ya mteja. Kwa kawaida msoma dira akisha soma ujumbe mfupi (sms) unatumwa kwa mteja kumjulisha juu ya usomaji kwa mwezi husika. Ikiwa msomaji dira wa Mamlaka hajafika kusoma kuanzia tarehe 01 hadi 15 ya kila mwezi, tafadhali ripoti suala hili mara moja katika ofisi za Mamlaka kwa kupiga simu ya bure (0800110088) ili kuepuka bili kua kubwa wakati itakaposomwa miezi inayofuata.

Ikiwa mteja amekosea kufanya malipo ya maji na kwamba pesa imeenda kwa mteja mwingine, atapaswa kufika ofisini kueleza suala hili na ikithibitika kwamba ni kweli alifanya malipo kimakosa. Ataelekezwa kuandika barua ili kuomba fedha aliyolipa iingizwe kwenye account yake sahihi. Hata hivyo Mamlaka inasisitiza wateja kuwa makini sana wanapofanya malipo kwa kuangalia jina linalotokea wakati analipa kwa wakala au mtandao wa simu.

Bili inaeza kua kubwa katika mwezi Fulani kuliko miezi mingine kwa sababu zifuatazo:-

 1. Bomba linalodondosha maji kwa matone matone mfululizo
 2. Maji yanayovuja katika mtandao wa mabomba ya ndani (Internal Plumbing System).
 3. Kufua kwenye bomba na maji yakiwa yanaendelea kutiririka.
 4. Kupiga mswaki huku bomba la maji likiwa linaendelea kutoa maji. Watoto wafundishwe matumizi mazuri ya maji.
 5. Kutumia majisafi na salama kwa ajili ya kumwagilia bustani, maji ya umwagiliaji si rahisi kuyakadiria; inashauriwa kutumia kutumia ndoo kumwagilia (Watering can)
 6. Kuosha vyombo wakati maji yanaendelea kutiririka. Ni vyema kuchota maji na kuoshea pembeni.
Hivyo mteja anapaswa kuwa makini katika matumizi yake ya maji, na ikiwa bado mteja atahisi kua dira inashida, anashauriwa kupiga simu ya bure au kufika ofisini ya kanda husika.

Ikiwa mteja atasitishiwa huduma ya maji kwa sababu yoyote ile, huduma itarudishwa ndani ya siku 1 hadi 2 za kazi mara baada ya kulipia gharama za kurejesha huduma.

kiwa umeona mvujoa wa maji tunaomba utoe taarifa kwa kupiga simu ya Mamlaka bure (0800110088) au kwa kujaza fomu ya maelekezo inayopatika kwenye fomu kwa kubonyeza hapa