Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mbeya (Mbeya WSSA) ipo katika Jiji la Mbeya ikiwa na jukumu kuu la kutoa huduma ya majisafi na uondoaji wa majitaka katika Jiji la Mbeya. Mamlaka ilianzishwa mwaka 1998 kwa Sheria Na. 8 ya 'Water Works Act Cap 272' ya mwaka 1997, iliyofanyiwa marekebisho na Sheria Na.12 ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2009.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mbeya ipo katika daraja A. Hii ikimaanisha kuwa ina wajibu wa kugharamia shughuli zote za uendeshaji na matengenezo, kulipa mishahara ya watumishi wake na pia kuchangia kwenye miradi ya uboreshaji na upanuzi wa mitandao ya Majisafi na Usafi wa Mazingira.
DIRA (VISION)Kuwa Mamlaka Bora katika kutoa huduma endelevu za Majisafi na Usafi wa Mazingira Nchini Tanzania.
DHIMA (MISSION)Kutoa huduma bora na endelevu za majisafi na usafi wa mazingira zinazokidhi vigezo vya kitaifa na kimataifa kwa bei nafuu.
KAULIMBIU (SLOGAN)'Maji ni Uhai'
MKURUGENZI MTENDAJI
CPA. Gilbert Kayange
KURIPOTI MIVUJO NA WIZI WA MAJI
Ili kuripot mvujo wa maji (Mfano: bomba kupasuka n.k), kuripoti wizi wa maji au uharibifu wowote wa miundombinu ya maji, tafadhali piga simu ya Ofisi namba: 0800110088 bure au kupitia mtandao kwa kubonyeza hapa.